Tuliahidi, tumetekeleza: Tanzania Yaiongoza Dunia MASIKIDU

 

Tanzania leo imeiongoza dunia kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani (MASIKIDU) kwa matukio mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali duniani yakiongozwa na hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi uliopewa jina la mmoja wa waasisi wa lugha hiyo, Ukumbi wa Kimtaifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. 

Jijini Dar es Salaam na Dakar: Akiongoza hafla hiyo Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango, alipokea salaam za Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliyeko Dakar Senegal kwa kikao cha AU.

Maputo, Msumbiji: salaam kutoka kwa Rais Phillep Nyusi wa Msumbuji nazo zilipambanhadla ya Dar es salaam.

Bujumbura, Burundi: Rais Ndaishimana wa Burundi naye pia aliwasilisha salaam zake kwa Kiswahili akiwatakia kheri Watanzania wenye Kiswahili chao.


Beijing: Nchini China mjadala mzuri wa Kiswahili uliohusisha wataalamu mbalimbali wa Kichina wanaozungumza Kiswahili umefanyika ukiratibiwa na Ubalozi.

New Yotk. Jijini NY, Marekani, kwenye makao makuu ya UN, Ubalozi wa Tanzania umeziongoza nchi nyingine kuadhimisha Siku ya Kiswahili. 

Paris: Vivyo hivyo jijini Paris, Ufaransa, makao makuu ya Unesco nako umefanyika mjadala mkubwa ambapo salaam maalum za Tanzania zimezolewa na Waziri wa Utamaduni Zanzibar, Tabia Maulid, huku msanii wa ngoma za asili kutoka Tanzania, Mrisho Mpoto akikonga nyoyo za wengi katika jiji hilo la Paris.



Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AWAPA SALAMU TEMBO WARRIORS, MHE. MCHENGERWA ATOA AHADI NONO WAKISHINDA

Mhe. Mchengerwa awakabidhi kombe la UEFA mashabiki wa Real Madrid

Waziri Mchengerwa azindua zoezi la kitaifa la kusaka na kuibua vipaji "mtaa Kwa mtaa."