Mhe. Mchengerwa amwakilisha Rais Samia msiba wa Bi. Hindu

 

Na John Mapepele

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia  Suluhu Hassan leo Julai 10, 2022 ametoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa  msanii  mkongwe wa Filamu nchini Chuma Seleman maarufu kama Bi. Hindu.

Salamu hizo zimetolewa kwa niaba yake na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe,  Mohamed Mchengerwa Magomeni jijini Dar es Salaam  nyumbani kwa marehemu kabla ya kwenda kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Akimzungumzia marehemu, Mhe. Mchengerwa amesema, Mhe. Rais amemwelezea   Bi. Hindu kuwa ni msanii aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia ya Sanaa hapa nchini.

"Bi Hindu ametoa  elimu ya sanaa kwa wasanii wengi sana, Serikali inatambua mchango wake. Mhe Rais amepokea msiba huu kwa msiba huu kwa mshituko mkubwa". Amefafanua Mhe, Mchengerwa

Aidha, amesema marehemu Hindu amefariki wakati Serikali inafanya mapinduzi makubwa  katika sekta za Sanaa.

Katika msiba huo Katibu Mwenezi wa CCM komrade Shaka na viongozi mbalimbali wa Serikali, Michezo na Sanaa wamehudhuria.


Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AWAPA SALAMU TEMBO WARRIORS, MHE. MCHENGERWA ATOA AHADI NONO WAKISHINDA

Mhe. Mchengerwa awakabidhi kombe la UEFA mashabiki wa Real Madrid

Waziri Mchengerwa azindua zoezi la kitaifa la kusaka na kuibua vipaji "mtaa Kwa mtaa."