MH. MCHENGERWA AIPONGEZA SIMBA KUINGIA ROBO FAINALI SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU AFRIKA
Na. John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza
timu ya Simba kwa kufuzu kuingia robo fainali ya ya Mashindano ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika baada ya kuibamiza vibaya timu ya
US Gendarmerie 4-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam
usiku wa kuamkia leo.
Mhe.
Mchengerwa ametoa pongezi hizo muda mfupi baada ya kumalizika kwa
mpambano huo ambapo amesema ushindi huo ni ushindi wa kihistoria.
"Ninaipongeza
Timu ya Simba kwa ushindi wa kishindo kuelekea kwenye Robo Fainali ya
Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika. Kama Taifa,
tunajivunia kwa ushindi huo mnono unaoitangaza Nchi yetu kimataifa."
Amefafanua Mhe. Mchengerwa
Ameitaka
Timu ya Simba kufanya maandalizi ya kutosha ili kuweza kufanya vizuri
zaidi katika mashindano hayo hatimaye kuchukua kombe na kuendelea
kuitangaza Tanzania duniani.
Simba
kwenye michuano ya robo fainali inaweza kukutana na TP Mazembe(DR
Congo), Orlando Pirates ( Afrika Kusini) na Al Ahly Tripoli (Libya).
Ukiachilia
timu hizi nne(4) timu nyingine nne(4) ambazo zimefuzu kuingia robo
fainali ya mashindano haya ni pamoja na RS Berkane (Morocco), Pyramids
(Misri), Al-Ittihad (Libya) na Al Masry Misri.
Simba inatarajiwa kuanzia nyumbani Uwanja wa Mkapa.








Comments
Post a Comment